Nchi nyingi washirika wa wengi wa NATO Alhamisi zimeelezea uungaji mkono wa mpango wa kuongeza matumizi ya ulinzi, huku wakisisitiza haja ya Ukraine na mataifa mengine ya Ulaya kuwa sehemu ya mazungumzo ya kumaliza vita vya Russia dhidi ya Ukraine.
Watu wenye silaha mashariki mwa Kongo waliwabaka mamia ya watoto na kuwaandikisha wapiganaji watoto katika viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto, UNICEF lilisema Alhamisi.
Mwandishi wa habari wa chombo cha habari dada cha VOA, Radio Free Europe/Radio Liberty, aliachiliwa kutoka Belarus Jumatano baada ya kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu. Kesi yake ilionwa na wengi kama iliyochochewa kisiasa.
Rais wa Liberia Joseph Boakai, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi uliokithiri, Jumatano aliwasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali walioteuliwa kwa kushindwa kutangaza wazi mali zao.
Vyuo vikuu vya umma vya Malawi vimeamuru wanafunzi wote wanaofadhiliwa na USAID waondoke au watafute njia mbadala za kulipia ada iwapo wangependa kuendelea na masomo.
Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir Jumatano limesema kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefunga anga yake kwa ndege zake zote, huku mzozo mashariki mwa DRC ukiongezeka.
Rais Donald Trump Jumatano alitangaza kwamba yeye na Rais wa Russia Vladimir Putin wamekubaliana katika mazungumzo ya simu “kuanza mara moja” mazungumzo na kiongozi wa Ukraine ili kumaliza mzozo wa karibu miaka mitatu.
Rais wa Cameroon Paul Biya atatizmiza umri wa miaka 92 kesho alhamisi na kuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani.
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Uganda Dr. Kiiza Besigye yupo katika mgomo wa kutokula katika gereza la Luzira anakozuiliwa.
Vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vinatarajiwa kugubika mazungumzo kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii ambapo mwenyekiti mpya wa umoja huo anatarajiwa kuchaguliwa.
Hali ya hewa ya theluji, na mvua ya barafu kali inatarajiwa kuendelea katika sehemu kadhaa Katikati mwa Marekani, Appalachinaa na majimbo ya yaliyo Katikati mwa Atlantic.
Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov, amesema kwamba mkutano wa washirika wa nchi hiyo, unaofanyika Brussels leo Jumatano, unaangazia namna ya kutoa silaha zaidi kwa Ukraine, ikiwemo mifumo muhimu ya ulinzi.
Pandisha zaidi