Vikosi vya akiba vya Sudan (RSF) na washirika wake Jumapili wamekubaliana kuunda serikali ya pamoja, licha ya onyo kwamba hatua hiyo inaweza kuisambaratisha zaidi nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.
Wapiga kura wa Ujerumani wanachagua serikali mpya katika uchaguzi wa Jumapili uliotawaliwa na wasiwasi kuhusu kudorora kwa miaka mingi kwa uchumi mkubwa zaidi wa Ulaya, shinikizo la kuzuia uhamiaji na kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wa Ukraine na muungano wa Ulaya na Marekani.
Waziri wa ulinzi wa Israel, Jumapili amesema wanajeshi wataendelea kubaki katika sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na walozwezi ambapo Israel imefanya mashambulizi ya wiki nzima, huku ikisema inazidisha uchunguzi wake katika eneo la Palestina.
Myanmar na mshirika wake wa karibu Russia, walitia saini mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji katika eneo maalum la kiuchumi la Dawei, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bandari na kiwanda cha kusafisha mafuta, Wizara ya Maendeleo ya Uchumi ya Russia, imesema Jumapili.
Papa Francis, Jumapili alikuwa na fahamu lakini bado anapokea mtiririko wa juu wa oksijeni ya ziada kufuatia tatizo la kupumua na kuongezewa damu, kwani bado yuko katika hali mbaya kwa maambukizo tata ya mapafu, Vatican imesema.
Kremlin Jumapili imesifu mazungumzo kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Russia, Vladimir Putin, ikiwaita “marais wawili makini sana” na kuapa kuwa kamwe haitaachilia eneo lililotwaliwa mashariki mwa Ukraine.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia amesema maandalizi yameanza kwa mkutano wa ana kwa ana kati ya rais wa Marekani Donald Trump na Vladimir Putin wa Russia.
Rais wa Tunisia Kais Saied siku ya Jumamosi alitoa wito kwa sheria inayosimamia benki kuu kufanyiwa marekebisho, na hivyo kuzua wasiwasi kwamba benki hiyo itapoteza uhuru wake na uingiliaji wa moja kwa moja wa serikali katika sera za fedha.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Rais wa Kenya William Ruto walihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mazungumzo yao ya simu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Ijumaa.
Burundi inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu wakati zaidi ya watu elfu 40 wamekimbilia nchini humo katika kipindi cha wiki mbili wakitoroka vita mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa umesema Ijumaa.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), Wafula Wanyonyi Chebukati, aliaga dunia jana Alhamisi katika hospitali moja mjini Nairobi akiwa na umri wa miaka 63, baada ya kuugua kwa muda mrefu, kama ilivyothibitishwa na familia yake.
Pandisha zaidi