Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 00:00

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Rais wa Kenya William Ruto wahimiza kusitishwa mapigano DRC


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akipanda ndege kuelekea Marekani, mjini Abu Dhabi, Falme za Kiara AP)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akipanda ndege kuelekea Marekani, mjini Abu Dhabi, Falme za Kiara AP)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na Rais wa Kenya William Ruto walihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa mazungumzo yao ya simu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Ijumaa.

Kusonga mbele kwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kumeashiria ongezeko kubwa zaidi katika zaidi ya muongo mmoja wa mzozo wa muda mrefu mashariki mwa Congo, uliotokana na ksambaa kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 nchini Congo na mapambano ya kudhibiti rasilimali kubwa ya madini ya nchi hiyo.

Rwanda inakanusha madai kutoka Congo, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi kwamba inaunga mkono kundi la M23 kwa silaha na wanajeshi.

Forum

XS
SM
MD
LG