Donald Trump ameapishwa leo Jumatatu kuchukua rasmi hatamu za uongozi kama rais wa 47 wa Marekani. Kurejea kwake madarakani ni tukio la kihistoria kwa mtu ambaye katika kipindi cha zaidi ya miaka tisa alikibadili chama cha Republican katika nchi inayozidi kukumbwa na migawanyiko.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump Jumapili amewahutubia maelfu ya wafuasi wake kwenye jiji kuu la Marekani Washington akiwaahidi kuchukua hatua kali dhidi ya uhamiaji.
Rais mteule Donald Trump, Jumapili amesema anapanga kutoa amri ya kiutendaji ambayo itaipatia kampuni mama ya mtandao wa TikTok, yenye makao yake China muda zaidi wa kutafuta mnunuzi aliyeidhinishwa kabla ya mtandao huo maarufu wa video kukabiliwa na marufuku ya kudumu ya Marekani.
Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumapili amemsamehe mzalendo mweusi Marcus Garvey, ambaye alimshawishi Malcolm X na viongozi wengine wa haki za kiraia ambaye alipatikana na hatia ya ulaghai wa barua katika miaka ya 1920.
Usitishaji mapigano uliokuwa ukitarajiwa kati ya Israel na Hamas umeanza baada ya kucheleweshwa kwa karibu saa tatu wakati Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliposema kuwa hautaanza isipokuwa Hamas itatoa orodha ya mateka watatu waliopangwa kuachiliwa Jumapili.
Kiongozi mkuu wa Taliban amekosoa hadharani sera ya serikali yake ya kupiga marufuku elimu kwa wanawake nchini Afghanistan, na kuiita chaguo binafsi badala ya tafsiri ya sheria za Kiislamu, au Sharia.
Mipango ya Thailand ya kuhalalisha uchezaji kamari mtandaoni inazua hofu kwamba magenge ya wahalifu yatatumia mwanya huo kuhamisha na kutakatisha fedha haramu kama walivyofanya na waendeshaji kamari katika nchi jirani.
Maelfu ya watu wengi wao wanawake waliandamana mjini Washington Jumamosi Disemba 18, 2025, kulalamika dhidi ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump, na kutoa ujumbe wa kulinda haki zote za kiraia na kibinadamu.
Zaidi ya wakimbizi wa ndani 55,000 wa Sudan wamerejea katika maeneo ya kusini mashariki mwa jimbo la Sennar, zaidi ya mwezi mmoja baada ya jeshi kutwaa tena mji mkuu wa jimbo hilo kutoka kwa wanamgambo, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji limesema Jumamosi.
Rais wa Korea Kusini, aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumamosi kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi muhimu ambayo itaamua kuhusu kuongeza muda wake wa kuzuiliwa huku wapelelezi wakichunguza maombi yake ya sheria ya kijeshi yaliyo shindikana.
Baraza la Mawaziri la Israel, Jumamosi limeidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza na kuachiliwa kwa mateka ambayo yatasimamisha vita vya miezi 15 na Hamas.
Serekali ya Sydney Jumamosi imetangaza janga la asili katika sehemu za mashariki mwa Australia ambako upepo umeangusha miti na kukata umeme kwa maelfu ya nyumba.
Pandisha zaidi