Hatua ya Marekani ya kuweka ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za chuma na aluminum zinazoagizwa kutoka nchi 35, ikiwemo Canada na nchi 27 wanachama wa EU ilianza kutekelezwa Jumatano.
Marekani ilifuta pia msamaha wa awali wa kutolipa ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Argentina, Australia, Brazil, Uingereza, Japan, Mexico na Korea Kusini.
“Kwa maoni yangu, marekebisho haya ni muhimu ili kushughulikia ongezeko kubwa la uagizaji wa bidhaa za chuma za zile zinazozalishwa kutoka kwenye chuma, ambazo zinatishia kudhoofisha usalama wa Marekani,” Trump alisema wakati akitangaza ushuru huo.
Canada iliweka papo hapo ushuru mpya kwenye bidhaa zinazouzwa nje na Marekani zenye thamani ya dola bilioni 27, huku Umoja wa Ulaya ukitangaza hatua ya ulipizaji kisasi kwa kuweka ushuru kwenye bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Marekani na mazao ya ukilima nchini Marekani. Hatua hiyo mpya ya EU inahusu bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 28.
Forum