Nje ya White House, ambako bendera zinapepea nusu mlingoti, Cheryl Jones wa Jimbo la California anasema Jimmy Carter alikuwa rais anayempenda.
Cheryl Jones, Mkazi wa California anasema: "Alikuwa mtu mzuri sana, mwenye heshima, muaminifu. Kitu ambacho hatukioni tena siku hizi."