Basi moja lilipinduka katika eneo la Johannesburg karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Afrika Kusini mapema Jumanne na kuua watu wasiopungua 12 maafisa wa mji huo wamesema huku wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Basi hilo lilikuwa limebeba zaidi ya watu 50 waliokuwa wanakwenda kazini wakati lilipoanguka katika barabara yenye shughuli nyingi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo, maafisa wamesema. Watu 12 waliuawa na wengine 45 kujeruhiwa, wamesema katika taarifa. Tumeishiwa maneno.
Hili ni janga, afisa wa usafiri wa mji wa Ekurhuleni Andile Mngwevu alisema. Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana mara moja. Ililazimisha kufungwa kwa barabara kuu inayoelekea uwanja wa ndege. Picha kutoka eneo la tukio zililionyesha basi hilo.
Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ameiambia televisheni ya Newzroom Afrika, kuwa inaonekana basi hilo lilikuwa likienda mwendo kasi.
Forum