Gavana wa Odesa, Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram vifusi vya Drone viliharibu majengo matano ya makazi.
Haya yanajiri mwaka mmoja baada ya serikali ya Sudan kusitisha uhusiano na jumuiya hiyo ya kikanda na kusitisha uanachama wake
Saa chache baadaye Wa-houthi walifyatua kombora katika uwanja wa ndege Ben Gurion na walirusha Drone kwenye mji wa Tel Aviv
Pyongyang imepeleka maelfu ya wanajeshi kuimarisha jeshi la Russia, ikijumuisha kwenye mkoa wa mpakani wa Kursk
Bunge lilipiga kura kutokua na imani na Scholz Desemba 16 baada ya serikali ya mseto ambayo ilisambaratika Novemba 6.
Rais wa Eritrea Asaias Afwerki, na mwenzake wa Somalia Sheikh Mohamud, Jumatano wamefanya mazunguzo ya kina yakiangazia ushirikiano pamoja na masuala ya kieneo yanayohusu mataifa yao.
Takriban watu 125 wameuawa nchini Msumbiji katika kipindi cha siku tatu za ghasia nchi nzima wakati wa maandamano yaliyoongozwa na upinzani dhidi ya matokeo ya uchaguzi, shirika lislo la kiserikali limesema siku ya Alhamis.
Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo ulikuwa mtupu Jumanne, siku ya mkesha wa Krismasi, huku kukiwa na ulinzi mkali katika vituo muhimu vya mji huo, siku moja baada ya mahakama ya katiba kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa Oktoba.
Raia wa Cameroon watapiga kura mwaka ujao kumchagua rais kwa muhula mwingine wa miaka saba. Chaguzi za awali katika taifa hili la Afrika ya Kati zilikumbwa na taarifa potofu ambazo zilichochea machafuko kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa kuenea kwa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii, waandishi wa habari nchini Msumbiji wako mstari wa mbele katika kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. Amarilis Gule ana ripoti kutoka Maputo, Idd Ligongo anaisoma ripoti kamili.
Pandisha zaidi