Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 19, 2025 Local time: 05:54

Mapato ya Botswana yaongezeka takriban mara mbili licha ya pingamizi lililowekwa na Uingereza


Ramani (Source - Google Maps)
Ramani (Source - Google Maps)

Msimu wa uwindaji, uliomalizika Novemba, ulifanyika huku kukiwa na upinzani unaoendelea kutoka baadhi ya nchi za Ulaya ambazo zinataka kuweka marufuku ya kusafirisha nyara za wanyama pori wa Afrika.

Botswana hutoa leseni takriban 400 za uwindaji tembo kila mwaka, na nyingi zikinunuliwa na wawindaji kutoka nje ya nchi.

Wynter Mmolotsi, waziri wa mazingira na utalii, ameliambia Bunge Alhamisi kuwa mamilioni ya dola zilipatikana kupitia mauzo zaidi yanayotokana na leseni za tembo katika maeneo ya vijiji vyenye wanayama pori.

“Ili kuweza kusimamia idadi ya wanyama pori, nchi hiyo inatekeleza mchanganyiko wa vyote utumiaji na kutotumia maliasili ya wanyama pori ili kupata faida ya kutosha ya kiuchumi, hasa kwa ajili ya jamii zetu.

Kwa mfano msimu wa uwindaji wa mwaka 2024, mgao wa jamii hiyo ulizalisha jumla ya fedha za Botswana pulas 42,863,423.

Pia, jumla ya pulas 15,633,950 zilipatikana kutokana na mauzo maalum ya fungu la tembo kusaidia hifadhi ya tembo na miradi inayoongozwa na jamii ndani ya eneo la tembo.

Mwaka 2023, Botswana ilijipatia dola milioni 2.7 kutokana na leseni za uwindaji.

Mmolotsi, hata hivyo anasema uwindaji huo unakabiliwa na upinzani wa nchi za Magharibi. Canada na Ubelgiji ni kati ya nchi ambazo hivi karibuni zilipiga marufuku uagizaji wa nyara za wanyama pori.



Forum

XS
SM
MD
LG