Idara kuu ya usalama ya Romania imesema Alhamisi kwamba inachunguza uwezekano wa kuingiliwa na mataifa ya nje kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili.
Sitisho la mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon lilianza kutekelezwa mapema Jumatano na hivyo kusimamisha mapigano ambayo viongozi wa Marekani na Ufaransa walisema yanaweza kufungua njia ya kuelekea kwenye sitisho jingine huko ukanda wa Gaza.
Israel Jumanne jioni imekubali kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, hatua ambayo huenda ikamaliza vita vilivyodumu kwa mwaka mmoja, iwapo sitisho hilo litaanza kutekelezwa Jumatano.
Ninatoa wito nchi wanachama kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wanafuata mkataba wa kimataifa unaopiga marufuku mabomu
Mamlaka ya Bandari, Bahari, na Mto Madagascar (APMF) imesema boti hizo zilisafiri kutoka Somalia kuelekea eneo la Ufaransa.
Maelfu ya wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan, Jumapili wameandamana kuelekea Islamabad wakiitishia kuachiliwa kwake pamoja na wafungwa wengine wa kisiasa.
Zvi Kogan mwenye miaka 28 kiongozi wa Orthodox alipotea Alhamisi alikuwa na duka la vyakula vya Kosher mjini Dubai.
Masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa ikijumuisha masuala ya Palestina na Lebanon pamoja na suala la nyuklia yatajadiliwa.
Kenya ilisisitiza haihusiani na kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani na mkosoaji wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Adani inaeleza hakuna athari za kibiashara kwa ripoti ya vyombo vya habari kwa shughuli za kampuni hiyo yenye makao yake India.
Chama cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na washirika wake wanatazamiwa kurejea mamlakani katika jimbo tajiri zaidi la taifa hilo
Mamia ya wanaharakati wa mazingira waliandamana siku ya Jumamosi katika mji wa Busan Korea Kusini kudai kuwa na ahadi kubwa zaidi za kimataifa za kupambana na taka za plastiki.
Pandisha zaidi