Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 01:00

UN yasema hali ya usalama Haiti inazidi kuwa hatari


Picha maktaba ya hali baada ya ghasia kati ka raia, Polisi , na makundi ya magenge kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince
Picha maktaba ya hali baada ya ghasia kati ka raia, Polisi , na makundi ya magenge kwenye mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince

Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, William O’Neil Jumanne ameambia wanahabari mjini New York kwamba hali ya kiusalama nchini humo ni tete huku akisihi wahusika wa kitaifa na kimataifa kuheshimu haki za binadamu.

Taifa hilo na limendelea kushuhudia ghasia za magenge, na Umoja wa Mataifa unakisia kwamba tayari magenge yamechukua udhibiti wa asilimia 85 ya mji mkuu wa Port-au-Prince. O’Neil alisema kuwa hali inazidi kuzorota zaidi kila anapotembelea taifa hilo. Alisema kwamba kutojali na ufisadi ni vizingiti vikuu katika kuvunja magenge hayo. Aliongeza kwamba serikali ya Haiti ni lazima iweke kipaumbele cha kumaliza maovu hayo mawili.

Ghasia za magenge nchini Haiti zimeendelea licha ya kuwepo kwa walinda usalama wa UN, wakiongozwa na kikosi cha Kenya. Afisa mmoja wa polisi wa Kenya alipigwa risasi mwezi uliopita wakati wa makabiliano na magenge. O’Neil alisema kwamba ameomba Marekani kubatilisha hatua ya kupokonya wahamiaji wa Haiti hati za muda za kuishi Marekani, ambazo kwa muda mrefu zimewaruhusu kuishi na kufanya kazi .

Mwezi uliopita, utawala wa Trump ulitangaza kuwapokonya hati hizo wahamiaji 500,000 wa Haiti na ambazo sasa muda wake wa mwisho ni Agosti mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG