Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 22:34

Watu wenye silaha waliivamia hoteli moja nchini Somalia


Ramani ya Somalia na miji yake.(Google map)
Ramani ya Somalia na miji yake.(Google map)

Kundi la Al Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake na lilisema limewaua zaidi ya watu 10. 

Watu wenye silaha waliivamia hoteli moja katika mji wa Baladweyne katikati mwa Somalia leo Jumanne ambako wazee wa eneo hilo pamoja na maafisa wa serikali walikuwa wanakutana na kuzingirwa kunaendelea, mashahidi na jamaa waliliambia shirika la habari la Reuters.

Dahir Amin Jesow, mbunge wa jimbo la Baladweyne, alisema hadi sasa kiasi cha watu wanne waliuawa lakini tunaendelea kuhesabu idadi ya vifo. Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake na lilisema limewaua zaidi ya watu 10.

Al-Shabaab mara kwa mara wanafanya mashambulizi ya mabomu na bunduki katika taifa hilo tete katika Pembe ya Afrika wakati likijaribu kuiangusha serikali na kuanzisha utawala wake kwa kuzingatia tafsiri yake kali ya sheria ya Kiislamu ya Sharia.

"Kwanza tulisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na milio ya risasi, kisha mlipuko mwingine ukasikika" alisema Ali Suleiman mfanyabiashara wa duka ambaye alishuhudia shambulio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG