Nchi hizo tatu, ambazo zina azma moja ya kukabiliana na kile wanachokiataja kama utawala wa Marekani, zimefanya mazoezi sawa katika eneo hilo katika miaka ya karibuni.
Mazoezi hayo yataanza Jumanne katika bandari ya Chabahar, iliyoko kusini mashariki mwa Iran kwenye Ghuba ya Oman, shirika la habari la Tasnim limesema, bila kutaja muda wao.
“Meli za kivita na zile za usaidizi za jeshi la wanamaji la China na Russia, pamoja na jeshi la wanamaji la Iran, na lile la Walinzi wa Mapinduzi,” chombo cha kiitikadi cha jeshi la Iran, kinatarajiwa kushiriki, kwa mujibu wa Tasnim.
“Mazoezi hayo yatafanyika kaskazini mwa Bahari ya Hindi na yanalenga kuimarisha usalama katika eneo hilo, na kupanua ushirikiano wa pande nyingi kati ya nchi zinazoshiriki,” Tasnim imesema.
Forum