Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 15, 2025 Local time: 11:46

Mamilioni ya Waafrika wako hatarini kupata kisukari - Utafiti


Watu wakijipatia chakula cha jioni katika jiji la Bamako huko Mali July, 5, 2016. Picha na VOA/ Roger Muntu
Watu wakijipatia chakula cha jioni katika jiji la Bamako huko Mali July, 5, 2016. Picha na VOA/ Roger Muntu

Utafiti mpya umebaini kuwa ugonjwa wa kisukari aina ya Type 2 unaongezeka kwa kasi miongoni mwa baadhi ya watu barani Afrika Kusimi mwa Sahara kuliko ilivyodhaniwa.

Watafiti wanaonya kuwa ugonjwa huo unaweza kuwaathiri mamilioni zaidi ya watu katika miongo ijayo kama vyanzo vinavyosababisha havitafanyiwa kazi.

Mlinzi Sibusiso Sithole, mwenye umri wa miaka 51, alipogunduliwa kuwa ana kisukari aina ya Type 2 miaka 13 iliyopita ilikuwa mshtuko kwake. Alikuwa akitembea maili sita kila siku kwenda na kutoka kazini kila siku , na hakudhani uzito wake ulikuwa ni tatizo. Mke wake ndiye aligundua kwanza mabadiliko ya afya yake.

Chumbani kwangu, niliona kuwa sikuwa sasa na nguvu za kutosha.

Tangu alipogundulika, Sithole alikuwa katika matibabu makali kwa ajili ya kisukari na shinikizo la damu.

“Ndiyo inabidi nichukue aina sita ya dawa kila siku”

Kisukari ni hali ambayo mwili unakuwa na tatizo kugeuza chakula kuwa nguvu kutokana na ukosefu wa insulini ya kutosha. Bila insulini, sukari hukaa kwenye damu badala ya kuingia kwenye seli, na hivyo kusababisha viwango vya juu vya sukari kwenye damu.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari lilikadiria mwaka 2021 kuwa watu wazima milioni 24 walio Afrika kusini mwa Sahara walikuwa wanaishi na hali hiyo.

Watafiti wanakadiria kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia sita au hata zaidi ya watu milioni 50, Waafika watakuwa na kisukari.

Utafiti uliochapishwa mwezi huu na jarida la afya la The Lancet linapendekeza asilimia halisi inaweza kukaribia mara mbili na ya awali iliyotabiriwa.

Forum

XS
SM
MD
LG