Mwanamuziki Beyonce Knowles hatimaye alipata tuzo ya albamu bora na rekodi yake ya muziki wa Country iitwayo 'Cowboy Carter' ambayo pia alishinda albamu bora ya muziki huo, tuzo ambayo alionekana kushtushwa kupokea huko Los Angeles California katika usiku wa tuzo za Grammy siku ya Jumapili.
Wanajeshi 14 kutoka Afrika Kusini wameuawa katika mzozo wa DRC na kuibua wito wa Afrika kusini kutaka kujiondoa
Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani, WHO, zitajadili kupunguza kwa sehemu ya bajeti yake, kwa dola milioni 400 kwa kuzingatia hatua ya Rais Trump kuiondoa Marekani, mfadhili wake mkuu, kutoka kwa shirika hilo,
Mamia ya majeruhi Jumatatu walionekana wakimiminika katika hospitali zilizojaa watu huko Goma, mji mkuu wa mashariki mwa Kongo, huku mapigano yakiendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao waliuteka mji huo wenye takriban watu milioni 2.
Rwanda Jumapili imekubaliana na pendekezo la kufanyika kwa mkutano utakaosimamiwa na SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kujadili mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku Tanzania ikitangaza pia kwamba wanajeshi wake wawili waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumapili ameambia viongozi wa Panama kwamba China ina ushawishi hatari kwenye mrefeji wa Panama, na kwamba iwapo hilo halitabadishwa, basi huenda Marekani ikalazimika kuchukua hatua muhimu za kulinda haki yake ya kutumia mfereji huo.
Polisi wa Georgia Jumapili wamekamata watu kadhaa kwenye maandamano ya maelfu ya watu waliojitokeza kuitisha uchaguzi mpya wa bunge, huku wakifunga kwa muda barabara muhimu kwenye mji mkuu wa Tbilisi.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Jumapili amesema kuwa atazingatia kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Marekani, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuashiria kuwa angeweka ushuru wa juu kwa Ulaya.
Uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wa kuweka ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za China umekabiliwa na maoni mchanganyiko kutoka Beijing.
Rais wa mpito wa Syria, amefanya safari yake ya kwanza nje ya nchi Jumapili, kwenda Saudi Arabia katika hatua ambayo ni kujaribu kuashiria kuondoka kwa Damascus kutoka Iran kama mshirika wake mkuu wa kikanda.
Rais wa Russia, Vladimir Putin, amesema kupuuza jukumu la Muungano wa Sovieti katika kukomboa kambi za kifo za Kinazi wa Wajerumani kama vile Auschwitz, na kutowaalika wanafamilia waliosalia wa wanajeshi wa Sovieti kwenye kumbukumbu za ukombozi ni kitendo cha aibu.
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jumapili limesema wanajeshi wake wawili wameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Pandisha zaidi