Ahmad al-Sharaa, ambaye wakati fulani alifungamana na al-Qaida, aliwasili Riyadh pamoja na waziri wa mambo ya nje wa serikali yake, Asaad al-Shaibani.
Wawili hao walisafiri kwa ndege ya Saudia, huku bendera ya Saudi Arabia ikionekana kwenye meza nyuma yao.
Televisheni ya taifa ya Saudia ilipongeza ukweli kwamba safari ya kwanza ya kimataifa ya al-Sharaa, inayotambulika imefanyika kwenda Riyadh.
Bendera mpya ya Syria yenye nyota na rangi tatu ilipepea karibu na ile ya Saudi Arabia kwenye uwanja wa ndege huku al-Sharaa akiwa amevalia suti na tai akishuka kutoka kwenye ndege.
Alipangiwa kukutana na Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman, mtawala mkuu wa ufalme huo, katika safari hiyo.
Forum