Wachambuzi wa mambo wanasema kwamba Kundi la wanamgambo la Sudan -RSF limeanza kupoteza nguvu dhidi ya jeshi la taifa kutokana na makosa ya mikakati, ugomvi wa ndani kati ya viongozi wake na kupungua vifaa.
Rubio alikuwa nchini El Salvador kwa mazungumzo na Rais Nayib Bukele na alitangaza kuwa Bukele alikubali kupokea wahamiaji kutoka Marekani
Maafisa wa huduma za dharura wa Israel wamesema watu wasiopungua sita wamejeruhiwa wakiwemo wanajeshi wawili.
Wakati huo huo jeshi la Ukraine limesema ulinzi wake wa angani ulitungua ndege 37 kati ya 65 zisizokuwa na rubani za Russia.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatatu amesitisha kwa muda ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada zinazoingia hapa Marekani kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuzungumza na rais wa Mexico Claudia Sheinbaum na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.
Mapigano makali huko kusini na magharibi mwa Sudan yaliua watu 65 na kujeruhi wengine zaidi ya 130 Jumatatu, madaktari wamesema, huku vita vibaya kati ta jeshi na kundi la wanamgambo vikipamba moto tena.
Uganda Jumatatu imeanza kutoa chanjo za Ebola aina ya Sudan, ugonjwa ambao umeua mtu mmoja na kutangazwa kuwa mlipuko wiki iliyopita.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem Jumatatu ameondoa ulinzi dhidi ya kurejeshwa nyumbani kwa mamia ya watu wa Venezuela waliopo Marekani, ikiwa sehemu ya mpango wa Trump dhidi ya uhamiaji haramu.
Muungano wa waasi wa Mashariki mwa Kongo unaojumuisha kundi la M23 umetangaza sitisho la mapigano kwa sababu za kibinadamu kuanzia Februari 4, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Mwanamuziki Beyonce Knowles hatimaye alipata tuzo ya albamu bora na rekodi yake ya muziki wa Country iitwayo 'Cowboy Carter' ambayo pia alishinda albamu bora ya muziki huo, tuzo ambayo alionekana kushtushwa kupokea huko Los Angeles California katika usiku wa tuzo za Grammy siku ya Jumapili.
Wanajeshi 14 kutoka Afrika Kusini wameuawa katika mzozo wa DRC na kuibua wito wa Afrika kusini kutaka kujiondoa
Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani, WHO, zitajadili kupunguza kwa sehemu ya bajeti yake, kwa dola milioni 400 kwa kuzingatia hatua ya Rais Trump kuiondoa Marekani, mfadhili wake mkuu, kutoka kwa shirika hilo,
Pandisha zaidi