Huku shinikizo likiongezeka kwa Israel na Hamas kuongeza muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano zaidi ya ilivyokua awali.
Kiwanda kinalenga kushindana na wazalishaji mafuta wa Ulaya wakati kinapoanza kufanya kazi kamili.
Uamuzi wa jaji Joseph N. Laplante wa New Hampshire umekuja baada ya hukumu mbili kama hizo kutolewa na majaji wengine wiki iliyopita.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili alisema anaamini Marekani imepiga hatua katika mazungumzo ya kumaliza vita kati ya Russia na Ukraine, lakini hakutoa maelezo yoyote kuhusu mawasiliano kati yake na Rais Vladimir Putin.
Mamlaka nchini Libya zilipata karibu miili 50 kwenye makaburi mawili ya watu wengi katika jangwa la kusini mashariki mwa nchi hiyo, maafisa walisema Jumapili.
Sam Nujoma ambaye aliongoza mapambano ya miongo mitatu ya kupigania uhuru wa Namibia kutokea Afrika Kusini yenye ubaguzi wa rangi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, ofisi ya rais ilitangaza Jumapili.
Hamas imewaachilia huru mateka wengine watatu wa Israel, Jumamosi kama sehemu ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano, hata wakati Rais wa Marekani, Donald Trump, anaendelea kuendeleza mpango wake wa kumiliki Ukanda wa Gaza.
Afrika Kusini, Jumamosi imekosoa uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, kusimamisha msaada kwa nchi hiyo kutokana na sheria aliyodai inaruhusu ardhi kunyakuliwa kutoka kwa wakulima wa kizungu.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na mwenzake wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, walishiriki mkutano wa Jumamosi, Tanzania, ambapo viongozi wa kikanda walitoa mwito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini DRC.
Rwanda ilisema Ijumaa kwamba ina ushahidi wa mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufanya shambulizi dhidi yake, na kukanusha kuwa ilikuwa ikichochea migogoro ndani ya mpaka wa nchi hiyo, jirani yake.
Utawala wa Trump umewasilisha mpango wa kupunguza wafanyakazi ulimwenguni kote, kwenye miradi inayopokea misaada kutoka Marekani, kama sehemu ya kulivunja shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, USAID, na kusalia na takriban wafanyakazi 300.
Zaidi ya maafisa wa polisi 100 wa Kenya waliwasili katika mji mkuu wa Haiti Alhamisi kuimarisha juhudi za kurejesha usalama za kikosi cha kimataifa ambacho mustakabali wake unatishiwa na hatua ya Marekani ya kusitisha sehemu ya ufadhili wake kwa kikosi hicho.
Pandisha zaidi