Watu wengi wanatuhumu polisi kwa kufanya vitendo hivyo lakini bado haijathibitishwa ni nani aliyehusika na utekaji huo.
Inaelezwa kuwa safari ya ndege ya Mahan Air ya Iran kuelekea Beirut ilifutwa kabla ya kupaa kwa sababu Lebanon haikutoa ruhusa ya kutua.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 amekuwa Papa tangu 2013 na amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya mara kadhaa.
Senegal imeanza kuzalisha aina mbalimbali za mafuta katika kiwanda chake cha kusafisha mafuta karibu na mji mkuu wa Dakar, kampuni iliyosafisha mafuta hayo ilisema Alhamisi.
Hamas Alhamisi ilisema itawaachilia mateka watatu zaidi wa Israel mwishoni mwa juma kama ilivyopangwa kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina.
Rais wa Marekani Donald Trump Alhamisi alisema kwamba Ukraine itashirikishwa katika mazungumzo ya amani na Russia, licha ya kuwa Kyiv imesema ni mapema mno kuzungumza na Moscow kwenye mkutano wa usalama leo Ijumaa.
Nchi nyingi washirika wa wengi wa NATO Alhamisi zimeelezea uungaji mkono wa mpango wa kuongeza matumizi ya ulinzi, huku wakisisitiza haja ya Ukraine na mataifa mengine ya Ulaya kuwa sehemu ya mazungumzo ya kumaliza vita vya Russia dhidi ya Ukraine.
Watu wenye silaha mashariki mwa Kongo waliwabaka mamia ya watoto na kuwaandikisha wapiganaji watoto katika viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto, UNICEF lilisema Alhamisi.
Mwandishi wa habari wa chombo cha habari dada cha VOA, Radio Free Europe/Radio Liberty, aliachiliwa kutoka Belarus Jumatano baada ya kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu. Kesi yake ilionwa na wengi kama iliyochochewa kisiasa.
Rais wa Liberia Joseph Boakai, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi uliokithiri, Jumatano aliwasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali walioteuliwa kwa kushindwa kutangaza wazi mali zao.
Vyuo vikuu vya umma vya Malawi vimeamuru wanafunzi wote wanaofadhiliwa na USAID waondoke au watafute njia mbadala za kulipia ada iwapo wangependa kuendelea na masomo.
Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir Jumatano limesema kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefunga anga yake kwa ndege zake zote, huku mzozo mashariki mwa DRC ukiongezeka.
Pandisha zaidi