Taarifa ya shirika hilo ilitolewa huku mzozo katika eneo hilo lenye utajiri wa madini ukizidi katika wiki za hivi karibuni.
"Katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini, tunapokea ripoti za kutisha za ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto unaofanywa na wahusika katika mzozo, ikiwa ni pamoja na ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia katika viwango vinavyozidi kitu chochote ambacho tumeona katika miaka ya hivi karibuni," Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell alisema katika taarifa yake.
Zaidi ya makundi 100 yenye silaha yanang’eng’ania udhibiti wa eneo lenye utajiri mkubwa wa madini la Kongo katika mzozo wa miongo kadhaa, ambao umezua mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani. Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda - kundi maarufu zaidi lenye silaha katika eneo hilo - waliteka Goma, mji mkubwa zaidi wa eneo, mwishoni mwa mwezi Januari katika ongezeko kubwa la mapigano ya miaka mingi, na vikosi vya serikali.
Forum