Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 15:25

Mkutano wa AU kuangazia vita DRC


Rais wa Rwanda President Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi, Apr. 29, 2024.
Rais wa Rwanda President Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi, Apr. 29, 2024.

Vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vinatarajiwa kugubika mazungumzo kwenye kikao cha Umoja wa Afrika kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii ambapo mwenyekiti mpya wa umoja huo anatarajiwa kuchaguliwa.

Mazungumzo kuhusu hali ya kibinadamu mashariki mwa DRC yataangaziwa zaidi.

Viongozi wa nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika wanatarajiwa kukutana Addis Ababa Ethiopia, wakati Afrika inakabiliwa na migogoro nchini DRC na Sudan, pamoja na hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kusitisha msaada kwa ajili ya maendeleo, jambo ambalo litaathiri sana bara hilo.

Mkutano wa dharura unatarajiwa kufanyika Ijumaa kujadili vita vya DRC, ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakiteka sehemu za mashariki mwa DRC kulipo na utajiri mkubwa wa madini.

Kundi la kufuatilia migogoro ya kimataifa – International crisis group, limesema kwamba vita vya DRC vinatishia kusababisha mvutano na mgogoro mkubwa kati ya nchi za maziwa makuu ilivyokuwa miaka ya 1990.

Forum

XS
SM
MD
LG