Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 17:14

DRC yafunga anga yake kwa ndege za Rwanda


Ndege ya shirika la Rwanda, RwandAir
Ndege ya shirika la Rwanda, RwandAir

Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir Jumatano limesema kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefunga anga yake kwa ndege zake zote, huku mzozo mashariki mwa DRC ukiongezeka.

Waasi wa M23 ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda walichukua udhibiti wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini mwishoni mwa mwezi Januari, kabla ya kusonga mbele kuelekea jimbo jirani la Kivu Kusini.

Mashambulizi ya waasi hao yamezorotesha zaidi uhusiano ambao tayari ulikuwa umeyumba kati ya nchi hizo mbili, na kuzua hofu kwamba nchi nyingine jirani huenda zikaingia kwenye mzozo mkubwa zaidi wa kikanda.

“Kufuatia hatua ya DRC ya kufunga anga yake kwa ndege za Rwanda, RwandAir imetafuta njia nyingine kwa ndege zilizoguswa na hatua hiyo,” shirika hilo lilisema katika taarifa.

“Tunafanya kazi ili kutoa huduma salama na zenye ufanisi zaidi huku tukijaribu kupunguza madhara kwa wasafiri wetu.”

RwandAir inafanya safari kwenye maeneo tofauti ya Afrika kama vile Johannesburg, Entebbe, Addis Ababa na Nairobi, pamoja na Brussels, London, Paris, Dubai na Doha, kulingana na tovuti yake.

Forum

XS
SM
MD
LG