Jumuia ya maendeleo ya Afrika Mashariki Jumatano ilionya kwamba mapigano ya hivi karibuni nchini Sudan Kusini yanaipeleka nchi hiyo “kwenye hatari ya kurudi katika vita.”
Serikali kuu ya Syria imefikia makubaliano na mamlaka inayoongozwa na Wakurdi ambao wanadhibiti eneo la kaskazini mashariki mwa nchi, ikiwa ni pamoja na sitisho la mapigano na kushirikishwa katika jeshi la Syria kwa kundi hilo linaloungwa mkono na Marekani.
Tanzania imeripoti visa vya kwanza vya ugonjwa wa Mpox, wizara ya afya ilisema Jumatatu, ikiwa ni mara ya kwanza virusi hivyo kugunduliwa katika mlipuko uliokumba nchi kadhaa za Afrika.
Serikali ya Thailand imesema Alhamisi kwamba inafanya majadiliano na maafisa wa serikali mbali mbali au maafisa wa balozi za nchi ambazo raia wao wamekwama kwenye mpaka kati ya Thailand na Myanmar.
Afrika Kusini inasema kwamba Marekani inajiondoa katika mpango wa kufadhili athari za mabadiliko ya hali ya hewa uliofikiwa na mataifa tajiri kuzisaidia nchi zinazoendelea kuachana na matumizi ya mkaa na kuanza kutumia nishati mbadala.
Zaidi ya Wakenya 60 waliookolewa kutoka mikononi mwa makundi ya matapeli wa mtandaoni nchini Myanmar wamekwama kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Thailand wakiishi katika mazingira mabaya, kulingana na taifa hilo la Afrika Mashariki.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Jumatano alisema mahakama za kimataifa zimeshindwa kukomesha ukatili wa miongo mitatu katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Zaidi ya wanamgambo 70 wa kundi la Al-Shabaab waliuawa nchini Somalia katika operesheni ya jeshi kwa ushirikiano na vikosi vya ndani, wizara ya habari ilisema Jumanne.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alisema kwamba “zaidi ya watu 7,000” wameuawa mashariki mwa nchi tangu mwezi Januari, wakati waasi ambao inasemekana wanaungwa mkono na Rwanda walipoteka miji miwili mikubwa.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Jumapili alisema uongozi mbaya wa mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi umechangia pakubwa kwa kuzidisha mzozo mashariki mwa nchi.
Juhudi za kuwaachilia mateka wanaoshikilia na wanamgambo wa Hamas, zinaendelea ili kuhakikisha kwamba wanaachiliwa wote wiki hii.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamewaua watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Watu 20 waliuawa Jumatatu kaskazini mwa Mali wakati magari waliyokuwa wakisafiria yaliposhambuliwa, huku vyanzo vya eneo hilo vikiiambia AFP kwamba mamluki wa Wagner na jeshi la Mali walihusika katika mauaji hayo.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ambaye alilazwa hospitali siku nne zilizopita akiwa na matatizo ya kupumua kutokana na mishipa ya kupitisha hewa kooni kuvimba, anakabiliana na hali ya afya isiyoeleweka.
Serikali ya Uganda Jumapili ilisema itaiondoa kesi dhidi ya mpinzani mkongwe Kizza Besigye katika mahakama ya kijeshi, na kumtaka asitishe mgomo wa kula gerezani, waziri mmoja amesema.
Senegal imeanza kuzalisha aina mbalimbali za mafuta katika kiwanda chake cha kusafisha mafuta karibu na mji mkuu wa Dakar, kampuni iliyosafisha mafuta hayo ilisema Alhamisi.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anaumwa sana akiwa jela siku tatu baada ya kuanza mgomo wa kula chakula.
Rais wa Liberia Joseph Boakai, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi uliokithiri, Jumatano aliwasimamisha kazi zaidi ya maafisa 450 wa serikali walioteuliwa kwa kushindwa kutangaza wazi mali zao.
Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir Jumatano limesema kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefunga anga yake kwa ndege zake zote, huku mzozo mashariki mwa DRC ukiongezeka.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wake mpya wa usalama na kumpandisha cheo mshirika wake kuwa makamu wa rais katika kile kinachohisiwa kuwa ni njia ya kumuandaa mrithi wake.
Pandisha zaidi