Hayo ni kulingana na maafisa wa Vatican ambao wamesema leo Jumatatu, wakiashiria kwamba kiongozi huyo wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka 88 huenda akaendelea kuwa hospitalini kwa muda zaidi kuliko ilivyotarajiwa.
Vatican imesema kwamba hotuba ya papa inayofanyika jumatano kila wiki haitafanyika.
Msemaji wa Vatican Matteo Bruni ameambia waandishi wa habari kwamba Papa Francis hata hivyo yuko sawa.
Mapema, Bruni alikuwa amesema kwamba Francis alikuwa na usiku mtulivu siku ya tatu hospitalini na kwamba alikula vizuri kiamsha kinywa na kusoma magazeti.
Matatizo ya mishipa ya koo yalipelekea Papa Francis kusitisha ziara yake Dubai, Desemba 2023 ambapo alikuwa amepangiwa kushiri mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa.
Papa Francis pia alifanyiwa upasuaji wa hernia, June 2023.
Alifanyiwa pia upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo mwaka 2021.
Amekuwa akitumia gari dogo la wagonjwa tangu mwaka 2022 kutokana na mauvimu ya kila mara ya goti na wakati mwingine huwa anatumia mkongojo kusimama.
Ameanguka mara kadhaa katika miezi michache iliyopita, na kupata majeraha kwenye mkono mwezi Januari, kando na kujeruhi jino mwezi Desemba alipoanguka kutoka kitandani.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ambaye alilazwa hospitali siku nne zilizopita akiwa na matatizo ya kupumua kutokana na mishipa ya kupitisha hewa kooni kuvimba, anakabiliana na hali ya afya isiyoeleweka.
Forum