Papa katika ujumbe wake amewataka waasi hao kuiongoza Syria kwa njia itakayohamasisha umoja katika taifa hilo.
Papa Francis amesema matumaini yake ni kwamba waasi hao wataiongoza Syria kwa njia itakayoleta suluhisho la kisiasa bila kuleta migogoro mingine, ubaguzi, kuwajibika na kuleta utulivu nchini humo.
Alikuwa akitoa hotuba yake ya kila wiki mjini Vatican. Hii ni mara ya kwanza amezungumzia hali ya Syria tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad.
Pia Papa ametoa wito kwa makundi ya kidini nchini humo kushirikiana kwa urafiki na heshima kwa ajili ya uzuri wa taifa la Syria.
Asilimia 90 ya watu nchini Syria ni Waislamu. Vatican inakadiria kwamba kuna wakatoliki 300,000 nchini Syria yenye jumla ya watu milioni 25.
Forum