Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:12

Jumuia ya Kimataifa yaomba makundi ya waliyo wachache kulindwa Syria


Picha ya wakimbizi wa Syria waliokimbilia Lebanon wakisubiri kurejea nyumbani. Picha ya maktaba.
Picha ya wakimbizi wa Syria waliokimbilia Lebanon wakisubiri kurejea nyumbani. Picha ya maktaba.

Maombi yanaongezeka kutoka kote duniani kuyalinda makazi na dini za walio wachache nchini Syria, kufuatia kuondolewa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad, na waasi wa Kiisalamu.

Wasi wasi mkubwa unalenga hasa kwa jamii ya Alawite, dhehebu ambalo familia ya Assad inatokea. Mapinduzi ya haraka yalipelekea kuchukuliwa kwa Damascus yakiongozwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham, au HTS, pamoja na makundi mengine ya waasi wa Kiislamu yanayoungwa mkono na Uturuki.

HTS ambalo limeorodheshwa na Marekani kama la kigaidi limeapa kulinda haki za jamii ya Alawite, pamoja na makundi mengine ya kidini ya waliyo wachache. Makundi ya kutetea haki yamesema kuwa ahadi hizo kwa kiasi kikubwa zimetekelezwa kufikia sasa. Hata hivyo, wasi wasi unaendelea kuhusu iwapo waasi watakaimarisha udhibiti katika nchi, pale watakapo chukua usukani.

Jamii ya Alawite ambao ni Waislamu wa dhehebu la Shia, ni takriban asilimia 10 ya wakazi milioni 24 wa Syria, wengi wao wakiwa kwenye majimbo ya pwani ya Latakia na Tatus, ingawa kuna idadi kubwa ya Alawite ambao pia wanaishi Damascus na Homs.

Tangu kuingia madarakani mwaka 1970, himaya ya Assad kwa kiasi kikubwa sana iliwategemea Alawite, ambao waliingia kujaza nafasi za juu katika jeshi na upelelezi.

Forum

XS
SM
MD
LG