Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:02

Kiongozi wa waasi akutana na Waziri Mkuu wa Syria ili kuzungumzia mpito


Kiongozi waupinzani wa Syria Abu Mohammed al-Golan.
Kiongozi waupinzani wa Syria Abu Mohammed al-Golan.

Kiongozi wa waasi nchini Syria Abu Mohammed al-Golani kwa mara ya kwanza Jumatatu  amekutana na waziri mkuu anayeondoka madarakani kufuatia kusonga mbele kwa  haraka kwa waasi ambao walimuondoa rais Bashar al Assad.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa waasi wa Telegram, Golani alikutana na waziri mkuu Mohammed Ghazi Jalali, ili kuratibu makabidhiano ya madaraka. Jalali Jumatatu ameiambia televisheni ya Sky News Arabia kuwa wanafanya hivyo ili kipindi cha mpito kiwe cha haraka na kisicho na tatizo.

Amesema kuwa mawaziri wengi bado wanafanya kazi zao kwenye ofisi zilizopo mjini Damascus. Hata hivyo mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Syria Adam Abdelmoula, ameliambia shirika la habari la AP kwamba baadhi ya huduma muhimu za serikali zimefungwa, huku wafanyakazi wa serikali wenye wasi wasi wakibaki nyumbani.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ombi la Russia lilikutana kwa faragha Jumatatu ili kujadili hali ya Syria. Russia imemsaidia Assad kijeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kwa takriban miaka 14.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir Pedersen, na mkuu wa ulinzi wa amani wa UN wote walitoa maelezo kwenye kikao hicho cha faragha. Kulikuwa na maswali mengi Jumatatu kuhusu ni nani ataiongoza nchi, na jinsi itakavyojaribu kujijenga baada ya vita vya miaka mingi na zaidi ya miongo mitano chini ya utawala wa familia ya Assad.

Forum

XS
SM
MD
LG