Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Jumatano ametupilia mbali wazo la kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu mkataba wa nyuklia, baada ya kupokea barua kutoka kwa Rais Donald Trump ambaye alipendekeza mazungumzo hayo.
Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 yataanza katika mji mkuu wa Angola tarehe 18 Machi, ofisi ya rais wa Angola ilisema Jumatano katika taarifa.
Angola Jumanne ilisema itajaribu kuanzisha katika siku zijazo mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 ambao inasemekana wanaoungwa mkono na Rwanda.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne alasiri alibadili msimamo kuhusu tishio lake la kuongeza maradufu ushuru kwenye chuma na aluminum kutoka Canada.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema leo Jumatatu haijapokea barua kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mazungumzo ya makubaliano ya nyuklia.
Mark Carney, ambaye hivi karibuni atakuwa waziri mkuu mpya wa Canada, ni gavana wa zamani wa benki kuu ya Canada na ile ya Uingereza, atakabiliwa na kibarua kigumu cha kuiongoza Canada chini ya ushuru wa ziada uliowekwa na Rais Donald Trump.
Maafisa wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump wamemkamata mwanafunzi raia wa Palestina aliyehitimu ambaye alihusika sana katika maandamano ya Wapalestina ya mwaka jana katika chuo kikuu cha Columbia cha New York, chama cha wanufunzi kilisema Jumapili.
Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika ,(CDC Africa) kimesema Alhamisi kwamba wimbi jipya la maambuziki ya Ebola limezuka Uganda na kwamba juhudi zinafanywa ili kuongeza ufuatiliaji wa maambukizi.
Wachambuzi wa siasa katika Umoja wa Ulaya wameonya kwamba itakuwa vigumu sana kwa umoja huo kuziba pengo la msaada wa ulinzi kwa Ukraine baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha msaada huo kwa Kyiv na kuonyesha kuiunga mkono Russia.
Mgonjwa wa pili wa Ebola, mtoto mwenye umri wa miaka minne alifariki nchini Uganda, shirika la afya duniani (WHO) lilisema, likinukuu wizara ya afya ya nchi hiyo. Kufuatia kifo hicho, idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa sasa ni 10.
Marekani na Uingereza zinajadiliana kuhusu mkataba wa kibiashara kati ya nchi mbili, Rais wa Marekani Donald Trump aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Alhamishi akiwa pamoja na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer.
Marekani itawekeza hadi dola bilioni 1 kukabiliana na kusambaa kwa mafua ya ndege, pamoja na kuongeza uagizaji wa mayai kutoka nje katika juhudi za kupunguza bei ghali ya bidhaa hiyo, waziri wa kilimo Brooke Rollins alisema Jumatano.
Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco Jumatano aliwataka raia wa nchi hiyo kutofanya ibada ya kuchinja kondoo wakati wa siku kuu ya Eid al-Adha mwaka huu kutokana na kupungua kwa mifugo nchini humo kufuatia ukame wa miaka mingi.
Uingereza Jumanne ilisema itasitisha msaada wa nchi kwa nchi kwa Rwanda na kuweka vikwazo vingine vya kidiplomasia kwa Kigali kutokana na jukumu lake katika mzozo katika nchi jirani ya Kongo.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatatu alisema kwamba nchi yake haipingi kushirikishwa kwa Ulaya katika mazungumzo ya amani kati ya Russia na Marekani yenye lengo la kumaliza vita vya Ukraine.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu lilipitisha azimio lilioandikwa na Marekani siku ya kumbukumbu ya miaka mitatu ya uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, azimio ambalo linachukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika mzozo huo.
Mazungumzo na Israel kupitia wapatanishi kuhusu hatua zijazo katika makubaliano ya kusitisha mapigano yana masharti ya kuwaachilia wafungwa wa Kipalestina kama ilivyokubaliwa, afisa wa Hamas Basem Naim alisema Jumapili.
Waconservative nchini Ujerumani wameshinda uchaguzi wa taifa Jumapili lakini uchaguzi huo wenye kura zilizosambaratika umekipa chama cha mrengo mkali wa kulia cha Alternative for Germany (ADF) matokeo yake mazuri kwa kupata nafasi ya pili.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani Marco Rubio amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete antoniuo jana kuhusu kubuni njia ya kuumaliza kwa amani mzozo wa mashariki mwa DRC , Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zenye Uchumi mkubwa - G20 wanakutana Afrika Kusini leo Ijumaa kufuatia mivutano baina ya wajumbe kuhusu vita vya Ukraine na migogoro ya kibiashara.
Pandisha zaidi