Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 01:31

Mwanafunzi aliyeongoza maandamano dhidi ya Israel akamatwa na maafisa wa usalama wa Marekani


Mahmoud Khalil, mwanafunzi aliyeshiriki katika maandamano dhidi ya Israel katika Chuo kikuu cha Columbia. Picha ya AP
Mahmoud Khalil, mwanafunzi aliyeshiriki katika maandamano dhidi ya Israel katika Chuo kikuu cha Columbia. Picha ya AP

Maafisa wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump wamemkamata mwanafunzi raia wa Palestina aliyehitimu ambaye alihusika sana katika maandamano ya Wapalestina ya mwaka jana katika chuo kikuu cha Columbia cha New York, chama cha wanufunzi kilisema Jumapili.

Mwanafunzi huyo Mahmoud Khalil alikamatwa Jumamosi na maafisa wa wiraza ya Marekani ya usalama wa ndani kwenye makazi ya chuo kikuu, chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Columbia kilisema katika taarifa.

Kushikiliwa kwa Khalil inaonekana kama mojawapo ya juhudi za kwanza za Rais Trump, kutimiza ahadi yake ya kutaka kuwafurusha baadhi ya wanafunzi wa kigeni waliohusika katika vuguvugu la maandamano ya kuiunga mkono Palestina.

Shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel na shambulizi lililofuata la Israel huko Gaza lilichochea miezi kadhaa ya maandamano ya Wapalestina katika vyuo vikuu vya Marekani.

Mke wa Khalil ni raia wa Marekani na Khalil ana kibali cha mkazi wa kudumu, chama cha wanafunzi kimesema.

Alikuwa mbaroni hadi Jumapili.

Forum

XS
SM
MD
LG