Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 23:17

Mfalme wa Morocco awataka wananchi kutofanya ibada ya kuchinja kondoo wakati wa Eid al-Adha


Mfalme wa Morocco
Mfalme wa Morocco

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco Jumatano aliwataka raia wa nchi hiyo kutofanya ibada ya kuchinja kondoo wakati wa siku kuu ya Eid al-Adha mwaka huu kutokana na kupungua kwa mifugo nchini humo kufuatia ukame wa miaka mingi.

Eid al-Adha itakayoadhimishwa mwezi Juni, inakumbusha kitendo cha Mtume Ibrahim, ambaye alikuwa tayari kumtoa kafara mtoto wake ili kutekeleza amri ya Mungu.

Waislamu wanaadhimisha siku kuu hiyo kwa kuchinja kondoo au mbuzi. Nyama hiyo inagawiwa kati ya familia na kutolewa kwa watu maskini.

“Ng’ombe na kondoo wa Morocco wamepungua kwa asilimia 38 mwaka 2025 tangu sensa ya mwisho miaka tisa iliyopita kutokana na misimu mfululizo ya ukame, kulingana na takwimu rasmi.

Forum

XS
SM
MD
LG