Hata hivyo Putin amebaini kwamba Brussels kwa muda mrefu imekuwa ikitupilia mbali majadiliano yoyote na Moscow.
Putin, ambaye alihojiwa na televisheni ya serikali ya Russia, alisema pia kwamba Rais wa Marekani Donald Trump anataka kusuluhisha mzozo wa Russia na Ukraine kwa kutumia busara na sio hisia.
Marekani na Russia walikuwa na mazungumzo ya awali kuhusu Ukraine wiki iliyopita nchini Saudi Arabia. Ukraine na washirika wa Kyiv hawakualikwa katika mazungumzo hayo, na pande hizo mbili zilipinga mchakato huo.
Putin alisema ni jambo la kueleweka kwa Ulaya kushirikishwa katika mazungumzo ya kumaliza mzozo huo wa miaka mitatu.
“Kushiriki kwao katika mchakato wa mazungumzo kunahitajika. Hatukuwahi kupinga hilo, tulifanya nao majadiliano mara kwa mara,” Putin alisema.
“Wakati fulani, kwa njama ya kutaka Russia ishindwe kwenye uwanja wa vita, wao ndio walikataa kuwasiliana nasi. Kama wanataka kurejea kwenye meza mazungumzo, ni sawa tu.”
Forum