Alisema mkataba kama huo unaweza kusaidia kuepusha Marekani kuiwekea ushuru Uingereza.
“Tutakuwa na mkataba bora wa kibiashara,” Trump alisema.
“Tutafikia mkataba mzuri wa kibiashara kwa nchi zote mbili, na tunalishugulikia hilo tunapozungumza hivi sasa.”
Starmer alisema nchi hizo mbili zimeanza kufanyia kazi mkataba mpya wa kiuchumi, unaozingatia teknolojia ya hali ya juu, ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara ambao tayari ulikuwa imara.
Trump alisema mambo ya msingi ya mkataba huo wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili washirika unaweza kufikiwa kwa “muda mfupi sana,” akisema waziri wake wa fedha Scott Bessent, Makamu wa Rais JD Vance, waziri wa biashara Howard Lutnick na mshauri wa usalama wa taifa Mike Waltz wataongoza juhudi hizo. Utasikia mengi zaidi kuhusu mkutano huo katika matangazo haya baadaye kidogo.
Forum