Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 23:19

Trump abadili msimamo kuhusu tishio lake la kuongeza maradufu ushuru kwa Canada


Rais Donald Trump baada ya kusaini amri ya kiutendaji kuhusu ongezeko la ushuru, Februari 13, 2025. Picha ya Reuters
Rais Donald Trump baada ya kusaini amri ya kiutendaji kuhusu ongezeko la ushuru, Februari 13, 2025. Picha ya Reuters

Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne alasiri alibadili msimamo kuhusu tishio lake la kuongeza maradufu ushuru kwenye chuma na aluminum kutoka Canada.

Trump alikuwa ameahidi kuongeza ushuru huo kutoka asilimia 25 hadi asilimia 50, na saa chache baadaye soko la hisa hapa Marekani lilitikiswa na tangazo la Trump.

Trump amebadili msimamo baada ya Gavana wa mkoa wa Canada wa Ontario kuachana na mpango wake wa kuongeza ushuru wa asilimia 25 kwenye umeme mkoa wake unaouza kwa wateja milioni 1.5 wa Marekani.

Hayo yakiarifiwa, Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na Warepublican Jumanne limepiga kura kuzuia uwezo wa Bunge kupinga kwa haraka ushuru uliowekwa na Rais Trump kwa nchi washirika wa kibiashara wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG