Russia imesema kwamba uhusiano wake na Marekani ni mbaya sana kiasi kwamba raia wake wameshauriwa kutosafiri kwenda Marekani, Canada au baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya.
Usafirishaji haramu wa binadamu umeongezeka sana kutokana na mizozo, majanga yanayosababishwa na hali ya hewa na mizozo ya dunia, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa Jumatano.
Sudan, kwa mwaka wa pili mfululizo imeorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayokumbwa na mzozo mbaya wa kibinadamu duniani katika ripoti iliyotolewa Jumatano na shirika la hisani la International Rescue Committee (IRC), ikifuatiwa na Gaza na Ukingo wa Magharibi, Myanmar, Syria na Sudan Kusini.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin Jumanne amethibitisha tena kile alichokiita uungwaji mkono usiotetereka wa ulinzi kwa Japan na Korea Kusini katika kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na China katika eneo la East China Sea.
Russia imesema kwamba vita vyake nchini Ukraine vitaendelea hadi malengo yake yaliyowekwa na rais Vladimir Putin yamefikiwa, iwe kwa njia ya kijeshi au mashauriano.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump Jumapili ametoa wito wa sitisho la haraka la mapigano na mazungumzo kati ya Ukraine na Russia ili kumaliza “vita visivyo na maana”, na kupelekea Rais Volodomyr Zelenskiy kusema amani haiwezi kupatikana bila dhamana.
Mashambulizi ya Israel huko Gaza yameua watu 20 Jumamosi, maafisa wa afya wamesema, huku Qatar ikielezea matumaini ya kasi mpya katika juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.
Waasi wa kikundi cha Hayat Tahrir al-Sham (HTS) wamesema walikuwa wameikamata miji ya Syria ya Talbis na Rastan.
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza msamaha kwa mtoto wake Hunter, ambaye angehukumiwa mwezi huu kwa makosa ya kumiliki silaha na kodi na huenda angehukumiwa kifungo cha miaka kadhaa.
Wanaharakati kutoka makundi mbalimbali ya mazingira ikiwa ni pamoja na Shirika la WWF na Greenpeace walikusanyika nje ya kituo cha maonyesho na mkutano wa mazingira mjini Busan wakitoa wito wa kupitishwa kwa mkataba wa plastiki wenye nguvu zaidi ili kukabili uchafuzi wa mazingira.
Kwa Nchi ya Kiafrika kuongoza kongamano kama la G-20, ingawa mwelekeo wake katika masuala kama vile ukuaji wa pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakahatarisha masuala magumu kama vile ushindani wa kibiashara na mivutano ya kidiplomasia.
Mashambulizi ya kijeshi ya Israeli yameua Wapalestina 17 katika Ukanda wa Gaza leo Alhamisi, madaktari wamesema, huku vikosi vikizidisha mashambulizi yao katika maeneo ya kati na vifaru kuingia zaidi kaskazini na kusini mwa eneo hilo.
Takriban watu 30 wanahofiwa kufariki baada ya maporomoko ya ardhi katika kijiji kimoja mashariki mwa Uganda, afisa mmoja wa eneo hilo alisema siku ya Alhamisi, akionya kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Mke wa mwanasiasa maarufu nchini Uganda Winnie Byanyima, ambaye mumewake alikamatwa katika nchi jirani ya Kenya amesema mwishoni mwa wiki kwamba hatarajii kuwa mume wake atapata haki katika mahakama ya kijeshi ambako ameshitakiwa.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameishutumu Marekani kwa kuongeza mvutano na uchokozi, amesema rasi ya Korea haijawahi kukabiliwa na hatari ya vita vya nyuklia kama sasa, shirika la KRT linalomilikiwa na serikali limesema.
Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema serikali yake ilikuwa inaongeza uwezo wa ulinzi wa anga.
Jeshi la polisi Afrika kusini -SAPS na maafisa wa jeshi wamesema juhudi za uokoaji kwa ajili ya wachimbaji madini waliokwama chini ya ardhi zinaendelea huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wa maisha yao.
Mwanasiasa maarufu wa upinzani wa Uganda alikamatwa wakati wa uzinduzi wa kitabu nchini Kenya mwishoni mwa wiki na kusafirishwa hadi Uganda, anashikiliwa katika jela ya kijeshi mjini Kampala, mke wake amesema leo katika mtandao wa kijamii wa X.
Kundi la viongozi wa zamani na wataalamu wa hali ya hewa wanasema mazungumzo ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya hali ya hewa hayafai tena kwa malengo yaliyoko.
Mamia ya wanafamilia waliokata tamaa kwa ajili ya ndugu zao wachimba madini haramu waliokwama kwenye mgodi Afrika Kusini wamemiminika nje ya mgodi huo wakisubiri kwa matumaini kuwa wapendwa wao watatoka chini ya ardhi.
Pandisha zaidi