Ofisi ya Netanyahu imeongeza kuwa Hamas inatarajia kuwaachilia mateka wa kwanza kwa mujibu wa makubaliano ya sitisho la mapigano linaloonza Jumapili.
Kama litafaulu sitisho hilo la mapigano litasimamisha mapigano ambayo yalikuwa katika sehemu kubwa za mjini zenye watu wengi huko Gaza, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 46 na kusababisha wengine takriban milioni 2.3 kukoseshwa makazi mara kadhaa, hiyo ni kulingana na mamlaka za ndani.
Huko Gaza pekee , ndege za kivita za Israel zimeendelea kufanya mashambulizi makali na huduma za kiraia za dharura zimesema leo takriban watu 101 ikiwemo wanawake 58 na Watoto wameuwawa tangu mpango huo wa sitisho la mapigano ulipotangazwa.
Forum