Botswana Jumatano inafanya uchaguzi wake mkuu ambapo Rais Mokgweetsi Masisi, anashindana na wagombea wengine watatu, akitafuta muhula wa pili kwenye taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa Almasi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza msaada wa dola milioni 135 zaidi kwa ajili ya wapalestina wakati wa ziara yake ya mashariki ya kati.
Polisi wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu wa msumbiji, Maputo Jumatatu walitumia gesi ya kutoa machozi wakati mamia ya watu wakiingia mitaani kupinga mauaji ya wakili wa upinzani.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahitaji kuchukua hatua zaidi ili kuongeza ufahamu kuhusu ugonjwa wa Mpox na upatikanaji wa chanjo.
Rais wa Kenya William Ruto Ijumaa alimteua waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kuwa naibu wake mpya, siku moja baada ya baraza la Seneti kupiga kura ya kumtimua naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua.
Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika, CDC, pamoja na wizara ya Afya ya Rwanda, Alhamisi wamesema kuwa kesi za maambukizi ya ugonjwa wa Marburg nchini humo zimeshuka.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sahara Magharibi, Staffan de Mistura ametoa wazo la kugawanywa kwa eneo hilo kati ya Morocco na Polisario Front, kama hatua ya kumaliza mzozo uliodumu kwa karibu miongo mitano
Bunge la seneti nchini Kenya Alhamisi lilipiga kura na kuidhinisha kuondolewa ofisini kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kutokana na mashtaka 5 kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake, katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa.
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi Jumatano ameteua Meja Jenerali Hassan Mahmoud Rashad, kuwa mkuu wa Idara yenye nguvu ya Intelijensia, akichukua nafasi ya Abbas Kamel ambaye sasa atakuwa mshauri wa Rais.
Ukamataji wa hivi karibuni hapa Marekani na Ulaya umepelekea maafisa wa usalama na idara za kijasusi kuwa macho na kuzua wasi wasi wa uwezekano wa kuinuka tena kwa kundi la kigaidi la Islamic State, dhidi ya mataifa ya Magharibi.
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman, na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, Jumanne wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, huku wakitoa wito wa sitisho la mapigano huko Gaza na Lebanon, wakati wa mazungumzo yao mjini Cairo.
Wakaazi wa mji mkuu wa Lebanon Beirut Jumanne wameendelea kuwa na wasiwasi baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutishia kuendelea na mashambulizi dhidi ya Hezbollah kote Lebanon pamoja na mji mkuu.
Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gashagua atakabiliana na Seneti katika kesi ya kutaka kuondolewa madarakani, baada ya mahakama ya juu mjini Nairobi, Kenya kukataa kutoa maagizo ya kuizuia Seneti kuendelea na mjadala.
Wizara ya Afya ya Zimbabwe Jumapili imethibitisha kesi mbili za kwanza za maambukizi ya mpox bila kueleza kwa kina aina kamili ya virusi hivyo.
Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema Jumapili kwamba waziri wa zamani wa Fedha na Kazi ambaye pia alikuwa gavana wa kwanza mweusi wa Benki Kuu, Tito Mboweni, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walizungumza Jumatano kuhusu mpango wa Israel wa kulipiza kisasi dhidi ya Iran, huku kundi la Hezbollah likisema wapiganaji wake waliwarudisha nyuma wanajeshi wa Israel kwenye eneo la mpakani.
Kampuni ya TikTok inakabiliwa na kesi mpya zilizowasilishwa Jumanne na majimbo 13 ya Marekani na jimbo la District of Columbia, yakiushtumu mtandao huo wa kijamii maarufu, kwa kudhuru na kushindwa kulinda vijana.
Kimbunga Milton kinaelekea Pwani ya Ghuba ya Florida, hapa Marekani, na kufikia dhoruba ya kiwango cha tano Jumanne, na kusababisha msongomano mkubwa wa magari na uhaba wa mafuta, huku maafisa wakiamuru zaidi ya watu milioni 1 kukimbia kabla hakijakumba eneo la Tampa Bay.
Meli yenye bendera ya Palau ilishambuliwa Jumatatu na kombora la Russia katika bandari ya kusini mwa Ukraine ya Odesa, kombora hilo liliua raia mmoja wa Ukraine na kujeruhi wahudumu watano katika shambulizi la pili kama hilo katika kipindi cha siku kadhaa, maafisa walisema.
Papa Francis atawateuwa makadinali wapya 21 kutoka duniani kote, alisema hayo Jumapili, katika hatua ambayo haikutarajiwa kushawishi kundi hilo lenye nguvu la watu wa kanisa ambao siku moja watamchagua mrithi wake.
Pandisha zaidi