Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 09:43

Shule ya Sudan iliyoko Libya yarejesha matumaini kwa watoto waliokoseshwa makazi


Watoto wa Sudan waliokoseshwa makazi wakiwa eneo la shule ambapo familia zao zimepewa hifadhi karibu na mji wa Gadaref katika nchi iliyotumbukia katika vita tangu Machi 6, 2024.
Watoto wa Sudan waliokoseshwa makazi wakiwa eneo la shule ambapo familia zao zimepewa hifadhi karibu na mji wa Gadaref katika nchi iliyotumbukia katika vita tangu Machi 6, 2024.

Shule moja ya Sudan iliyoko Libya imerejesha matumaini kwa watoto wengi waliokoseshwa makazi kuendelea na masomo yao kufuatia vita katika taifa lao na gharama ambazo hawawezi kuzimudu.

Shule ya Al- Takamul huko Misrata inawahifadhi takriban wanafunzi 512 waliokoseshwa makazi, baadhi yao o walikuwa nje ya shule kwa takriban miaka miwili.

Samah Mohamed alikimbia Sudan na Watoto wake sita akipita katika njia zisizo halali na kupata sehemu ya kufanya kazi na Watoto wake kusoma.

“ lengo langu la pili baada ya usalama ilikuwa ni elimu, n mshukuru Mungu nimefanikiwa.” Alisema Mohammed.

Shule hiyo pia inatoa elimu kwa Watoto wengi wenye mahitaji maalumu au wale ambao wameathirika kisaikolojia kutokana na vita.

Tahani Mohammed Saleh mama yake na Mohamed ambaye ana mahitaji muhimu ya kielimu alimwandikisha mtoto wake wa kiume baada ya kuathirika kisaikolojia , tatizo la kujikojola, khofu, na kupoteza hamu ya kula kwa sababu ya vita.

Forum

XS
SM
MD
LG