Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 04:24

Guterres analiomba baraza la usalama kutoa msaada wake kuwalinda raia wa Sudan


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. October 24, 2024. (Photo by Alexander Zemlianichenko / POOL / AFP)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. October 24, 2024. (Photo by Alexander Zemlianichenko / POOL / AFP)

Vita nchini Sudan vilizuka katikati ya April mwaka 2023 kufuatia mapambano ya madaraka kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha RSF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliomba baraza la usalama leo Jumatatu, msaada wake katika kuwalinda raia katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita, lakini amesema hali sio nzuri kupelekwa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa.

“Watu wa Sudan wanaishi na jinamizi la ghasia, huku maelfu ya raia waliuawa na wengine wengi wanakabiliwa na ukatili usioelezeka, ikijumuisha ubakaji ulioenea na unyanyasaji wa kingono”, Guterres aliliambia baraza hilo lenye wanachama 15.

Vita nchini Sudan vilizuka kati-kati ya April mwaka 2023 kutokana na mapambano ya madaraka kati ya Jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces, kabla ya mpango wa mpito kuelekea kwa utawala wa kiraia, na kusababisha mgogoro mkubwa zaidi wa makazi duniani.

“Sudan, kwa mara nyingine tena, inakuwa jinamizi la vurugu za umma za kikabila, alisema Guterres, akielezea mgogoro katika mkoa wa Darfur nchini Sudan, kiasi cha miaka 20 iliyopita na kupelekea Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Vita-ICC kuwafungulia mashtaka viongozi wa zamani wa Sudan, kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG