Paris na Rabat kwa miaka mingi wamekuwa na taharuki ya mahusino katika miaka 3 iliopita hasa kuhusiana na masuala ya uhamiaji pamoja na eneo linalozozaniwa na Sahara Magharibi, ambalo Morocco inashinikiza jumuia ya kimataifa kulitambua kama sehemu yake.
Wakati akichukua hatua makini ili kijiepusha kukasirisha Algeria ambaye ni hasimu wa Morocco, Macron alilazimika kuunga mkono Morocco kwenye suala la Sahara Magharibi hapo Julai, hatua iliofungua njia ya mardhiano. Macron anafanya ziara ya Morocco akiandamana na darzeni ya mawaziri pamoja na wafanyabiasha 40 mashuhuri kutoka Ufaransa.
Akionyesha heshima isiyo ya kawaida, Mfalme Mohamed wa 5, wakati akitembelea kijiti, alimlaki Macron akiwa na mke wake Brigitte kwenye uwanja wa ndege Jumatatu, kabla ya kuanza kwa hafla ya kutia saini mikataba kwenye kasri ya Mfalme. Shirika la reli la Morocco la ONFC, limetia saini mkataba na kampuni ya Ufaransa ya Alstom wa kununua mabehewa 12 ya mwendo kasi.
Forum