Mzozo huo ulioanza 1975 ni kati ya Morocco inayochukulia Western Sahara kuwa himaya yake na kundi la Polisario Front, linaloungwa mkono na Algeria, likiitisha kujitawala. Morocco kwa upande wake inasema kuwa inaweza tu kuruhusu eneo hilo kujitawala likiwa chini ya serikali yake, lakini Polisario Front limekuwa likiitisha kuwe na kura ya maoni kuelekea kujitawala kama nchi huru.
Wakati akizungumza faraghani mbele ya Baraza la Usalama la UN, de Mistura ambaye ni mwanadiplomasia wa siku nyingi kutoka Italy alisema kuwa ugawanyaji huo utaruhusu kubuniwa kwa taifa huru upande wa kusini, na kwa upande mwingine kuruhusu Morocco kuchukua sehemu iliyobaki ikitambuliwa kimataifa.
Aliongeza kusema kuwa licha ya pendekezo hilo. Wote Morocco na Polisario Front hawakuridhia. Alisema kuwa Katibu Mkuu wa UN anahitaji kutadhimini tena jukumu lake kama mjumbe maalum iwapo hakuna hatua zitakazokuwa zimepigwa kuelekea sululosho la mzozo huo ndani ya miezi 6.
Forum