Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 03:46

Mfalme wa Morocco awasamehe zaidi ya wakulima 4,800 wa bangi


Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita
Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita

Mfalme wa Morocco Mohammed wa Sita aliwasamehe zaidi ya wakulima 4,800 wanaoshtumiwa kulima bangi kinyume cha sheria, wizara ya sheria ilisema Jumatatu.

Mfalme “alitoa msamaha kwa watu 4,831 waliopatikana na hatia, kushtakiwa au kutafutwa katika kesi zinazohusiana na kilimo cha bangi,” wizara ya sheria ilisema katika taarifa.

Tangazo hilo limetolewa kabla ya likizo ya kitaifa leo Jumanne.

Morocco ni mzalishaji mkubwa zaidi wa bangi duniani, kulingana na Umoja wa Mataifa. Ilipitisha sheria mwaka 2021 kuhusu uzalishaji wa bangi na kuitumia kama matibabu, na kuruhusu kilimo cha bangi katika mikoa ya vijijini katika eneo la kaskazini mashariki la Rif.

Wakati ikiwa na lengo la kupiga vita biashara haramu, nchi hiyo inataka kujiweka kwenye soko la kimataifa la bangi halali ambayo imekuwa ikizalishwa katika eneo la Rif kwa karne kadhaa, ikitoa riziki kwa familia kati ya 80,000 na 120,000 mwaka 2019, kulingana na makadirio rasmi.

Msamaha huo unalenga kuwaruhusu wahusika “kujumuika katika mkakati huo mpya”, kulingana na taarifa ya wizara ya sheria.

Morocco ilianzisha idara maalum, ANRAC, ili kuunda kilimo halali na usafirishaji wa bangi kwa madhumuni ya matibabu, dawa na viwanda.

Idara hiyo tayari imetoa vibali zaidi ya 200 vya kusindika bangi, kuagiza mbegu kutoka nje na kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi.

Forum

XS
SM
MD
LG