Wakati vyombo vya habari vya Israel vikiripoti kuwa baraza la mawaziri limeidhinisha pendekezo la sitisho la mapigano.
Akiungumza na Waandishi wa habari, mkuu wa ofisi ya Habari ya Hezbollah Mohammad Afif amesema
“Kurejea kwa rais mteule Donald Trump katika urais, na katika kipindi cha miezi mwili kabla ya ya kuchukua rasmi madaraka ya urais, kumekuwa na shughuli nyingi kati ya Washington, Moscow, Tehran, na katika miji mikuu kadhaa.”
“Kuna mazungumzo mengi kwenye vyombo vya habari, Mawazo ya ksiiasa na juhudi. Tunasiki mazungumzo mengi, lakini mpaka sasa, kulingana na taarifa zangu, hakuna kilicho rasmi kilichoifikia Lebanon au sisi kuhusiana na suala hili.”aliongeza
Naye Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Gideon Saar amesema siku ya Jumatatu kuwa kuna maendeleo yamepatikana katika mazungumzo ya sitisho la mapigano lakini utekelezaji umebaki kuwa kipengele muhimu.
Yedioth Ahronoth, gazeti linalouzwa zaidi nchini Israel, limeripoti siku ya Jumatatu kuwa Israel na Lebanon wamekuwa wakibadilishana rasimu kupitia mjumbe wa Marekani Amos Hochstein, ikiashiria maendeleo ya jitihada za kufikia makubaliano.
Forum