Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:57

Wapatanishi wa Marekani kwenye juhudi za kuleta sitisho la mapigano kati ya Israel na Hezbollah


Moshi ukipaa angani kutokana na shambulizi la Israel dhidi ya kijiji cha kusini mwa Lebanon cha Khiam, Oktober 30, 2024.
Moshi ukipaa angani kutokana na shambulizi la Israel dhidi ya kijiji cha kusini mwa Lebanon cha Khiam, Oktober 30, 2024.

Wapatanishi wa Marekani wanafanyia kazi pendekezo la kusimamisha vita kati ya Israel na kundi lenye silaha la Hezbollah nchini Lebanon, kwa kuanzisha sitisho la siku 60, vyanzo viwili vimesema Jumatano.

Hata hivyo, Israel iliendelea na mashambulizi yake kwa kuwaamuru wakazi wa mji wa mashariki mwa Lebanon, Baalbek, kuhama. Vyanzo hivyo – ambapo mmoja alipata maelezo juu ya mazungumzo na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu anayeshughulika na masuala ya Lebanon, ameiambia Reuters kuwa kipindi cha miezi miwili kingetumiwa kukamilisha utekelezaji kamili wa Azimio la Baraza la Usalama la UN, nambari 1701, lililopitishwa 2006 kuhakikisha kwamba eneo la kusini mwa Lebanon linabaki huru na nje ya udhibiti wa serikali.

Jitihada hizo mpya zinakuja wakati operesheni ya Israel dhidi ya Hezbollah inayoungwa mkono na Iran nchini Lebanon ikiendela kuongezeka. Jeshi la Israel Jumatano lilitoa amri ya kwanza ya watu kuondoka mjini Baalbek, ambako maelfu ya raia wa Kiislamu wengi wakiwa wa dhehebu la Shia, ikiwa ni pamoja na wengi waliokimbia maeneo mengine, walikuwa wakiishi.

Mjumbe wa rais wa Marekani Amos Hochstein, ambaye anafanyia kazi pendekezo jipya la sitisho la mapigano, aliwaambia waandishi wa habari mjini Beirut mapema mwezi huu kwamba masharti bora ya utekelezaji yanahitajika wakati si Israel wala Lebanon wametekeleza kikamilifu azimio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG