Kundi la waangalizi wa uchaguzi wa mashirika ya kiraia msumbiji wamesema shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Bairro Da Coop karibu na mji mkuu Maputo , na kumuuwa wakili wa chama cha Podemos, Elvino Dias na mwakilishi wa chama paulo Guambe.
Chama kipya cha upinzani Podemos na mgombea wake wa urais Venancio Mondlane wamekataa matokeo ya muda yanayoonyesha uwezekano wa ushindi wa Frelimo chama ambacho kimetawala msumbiji kwa nusu karne , na mgombea wake ni Daniel Chapo.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa Oktoba 24 lakini kuna wasiwasi kwamba maandamano yanaweza kubadilika na kuwa na umwagaji damu.
Vikosi vya usalama vya msumbiji viliwahi kufyatulia risasi waandamanaji , ikiwemo baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana, hiyo ni kwa mujibu wa makundi ya haki.
Forum