Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 13:27

Daniel Chapo mgombea urais Msumbiji kwa chama tawala anayetarajiwa kushinda


Daniel Chapo, Mgombea urais wa chama tawala nchini Msumbiji
Daniel Chapo, Mgombea urais wa chama tawala nchini Msumbiji

Akifanya kampeni ikilenga “tufanye kazi” Daniel Chapo mwenye miaka 47 anatarajiwa kusimamia ujenzi wa miradi ya gesi asilia.

Mgombea kiti cha rais wa chama tawala nchini Msumbiji katika uchaguzi wa mwezi huu, ambaye ana uhakika wa kushinda huenda akaendelea kutegemea jeshi la Rwanda na fedha za Ulaya ili kupata viwanda vyake vikubwa vya gesi katika jimbo ambalo limekumbwa na ghasia zinazofanywa na kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali wa Kiislamu, wachambuzi wanasema.

Akifanya kampeni chini ya kauli mbiu “tufanye kazi”, mwalimu wa zamani wa shule ya msingi Daniel Chapo, mwenye miaka 47, anatarajiwa kusimamia ujenzi wa miradi miwili ya gesi asilia (LNG) ambapo kwa sasa hakuna kazi zinazofanyika kwa sababu ya ukosefu wa usalama katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.

Ili kufanikisha hilo, ni lazima ategemee sana jeshi la Rwanda lililoletwa na Rais wa sasa Felipe Nyusi mwaka 2021 ili kuimarisha vikosi vya ndani vinavyopambana.

Forum

XS
SM
MD
LG