Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 07:21

Mashambulizi yaliyofanywa na Israel yaua Wapalestina 47, darzeni wajeruhiwa


Israel yashambulia Nuseirat, katikati ya Ukanda wa Gaza
Israel yashambulia Nuseirat, katikati ya Ukanda wa Gaza

Wapalestina 47 wameuawa na darzeni kujeruhiwa, wengi wao wakiwa watoto na wanawake katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia Ijumaa yaliyotekelezwa na Israel katikati mwa ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la Palestina WAFA, limeripoti kwamba mashambulizi yametokea katika mji wa Deir Al-Balah, kambi ya Nuseirat, na katika mji wa Al-Zawayda.

Ramani ya Ukanda wa Gaza (Foto: AFP)
Ramani ya Ukanda wa Gaza (Foto: AFP)

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wamewalenga na kuwaua magaidi kadhaa waliokuwa wamejihami katikati mwa Gaza na kuua darzani kadhaa katika sehemu ya Jabalia, kaskazini mwa Gaza.

Vita vya Gaza vilianza baada ya wanamgambo wa Hamas kushambulia Israel Oktoba 7 2023 na kuua watu 1,200, kuteka nyara 251 na kurudi nao Gaza.

Mashambulizi ya Israel katika Gaza yameua zaidi ya wapalestina 43,000 na kuharibu kabisa sehemu hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG