Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:52

Makao ya Netanyahu yameshambuliwa


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Sept. 27, 2024.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Sept. 27, 2024.

Serikali ya Israel imesema kwamba ndege isiyokuwa na rubani Jumamosi ilishambulia makao ya waziri mkuu lakini hakuna mtu alijeruhiwa.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake hawakuwa nyumbani wakati wa shambulizi hilo.

Kiongozi wa juu zaidi wa Iran ameapa kwamba wanamgambo wa Hamas wataendelea kupigana dhidi ya Israel kufuatia mauaji ya kamanda wa mashambulizi ya Oktoba 7.

Watu 21 wameuawa katika ukanda wa Gaza kwenye mashambulizi kadhaa ya Israel. Kati ya waliofariki ni watoto.

Ving’ora vimelia jumamosi nchini Israel, vikionya uwezekano wa mashambulizi kutokea Lebanon.

Mnamo mwezi Septemba, waasi wa Houthi walirusha makombora ya masafa marefu kutoka Yemen, wakilenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion wakati ndege iliyokuwa imembeba Netanyahu ilikuwa inatua. Makombora yalinaswa.

Forum

XS
SM
MD
LG