Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:17

Wataalam wa mazingira wasema nchi zinazoendelea zinahitaji dola trilioni 1

Viongozi wanaoshiriki Kongamano la mazingira la COP29.
Viongozi wanaoshiriki Kongamano la mazingira la COP29.

Wataalam ambao wamezungumza katika kongamano la mazingira la mwaka huu COP29, wamesema nchi zinazoendelea zinahitaji dola trilioni 1 kila mwaka.

Kiwango hicho kinahitajika kufikia mwisho wa muongo huu, ili kuhakikisha kwamba kuna nishati safi na kujilinda dhidi ya hali mbaya ya hewa.

Suala la pesa linaangaziwa sana katika mkutano wa COP29 unaofanyika Azerbaijan na mafanikio ya mkutano huo yanaweza kuamuliwa kwa kuzingatia iwapo nchi zitakubaliana.

Makubaliano hayo ni kuhusu kiwango cha pesa nchi tajiri, washirika wa maendeleo na sekta binafsi zinastahili kutoa kila mwaka kwa nchi zinazoendelea kugharamia mabadiliko ya hali ya hewa.

Wanaharakati wakiwa wamebeba bango lenye maandishi "hakuna uadilifu wa hali ya hewa wakati damu ikiwa katika ardhi zetu" katika mkutano wa COP29, Alhamisi, Novemba 14, 2024, in Baku, Azerbaijan.
Wanaharakati wakiwa wamebeba bango lenye maandishi "hakuna uadilifu wa hali ya hewa wakati damu ikiwa katika ardhi zetu" katika mkutano wa COP29, Alhamisi, Novemba 14, 2024, in Baku, Azerbaijan.

Azimio la kuchangisha dola bilioni 100 kila mwaka, linalomalizika mwaka 2025, lilifikiwa miaka miwili baadaye mwishoni mwa mwaka 2022.

Hata hivyo kiasi kikubwa cha pesa hizo kilikuwa ni mikopo na wala sio pesa zisizokuwa na riba, jambo ambalo nchi zinazopokea zinasema linastahili kubadilika.

Forum

XS
SM
MD
LG