Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:00

Wanafamilia wa wachimba madini haramu wakusanyika nje ya mgodi


Mgodi wa Stilfontein, Afrika Kusini, Nov. 15, 2024.
Mgodi wa Stilfontein, Afrika Kusini, Nov. 15, 2024.

Mamia ya wanafamilia waliokata tamaa kwa ajili ya ndugu zao wachimba madini haramu waliokwama kwenye mgodi Afrika Kusini wamemiminika nje ya mgodi huo  wakisubiri kwa matumaini  kuwa wapendwa wao watatoka chini ya ardhi.

Wachimbaji wako katika mvutano na polisi ambao wamezuia kupelekewa chakula na maji, na wanajaribu kuwalazimisha kutoka ili wakamatwe kwa sababu ya kuingia kinyume cha sheria kwenye machimbo ulioachwa wakitafuta dhahabu zilizobaki , hili ni tatizo la kawaida Afrika Kusini.

Zaidi ya wachimbaji haramu 1000 tayari wametoka katika wiki za karibuni huku polisi wakiwakamata na kulikuwa na maiti moja iliyopatikana.

Haiko wazi kama wale waliobaki katika mgodi wa Stilfontein katika jimbo la NorthWest hawako tayari au hawakuweza kutoka nje ya shimo lenye urefu wa zaidi ya kilomita 2 chini ya ardhi.

Ndugu na marafiki wakishinikiza kuwepo mabadiliko katika mfumo wa uchambaji madini ya dhahabu katika mgodi ambao wachimbaji haramu wamekwama, Afrika Kusini, Ijumaa, Nov 15, 2024.
Ndugu na marafiki wakishinikiza kuwepo mabadiliko katika mfumo wa uchambaji madini ya dhahabu katika mgodi ambao wachimbaji haramu wamekwama, Afrika Kusini, Ijumaa, Nov 15, 2024.

Polisi na wana jumuiya walisimama karibu na mlango wa mawe kwenye sehemu ya kuingilia ambako kulikuwa na kifaa kilichowekwa kwa ajili ya kuwavuta nje wanaume hao.

Mwanafamilia Shona Roselina anasema: “ Ndio tunao wanafamilia zaidi ya 20 , waliokuja kutoka Chipinge nchini Zimbabwe. Tunatumai watatoka nje ili tuwapeleke nyumbani. Mmoja ana mke ambaye yuko hapa. Analia, hatujui jinsi ya kumsaidia. Mume wake alikwenda chini ya ardhi mwezi Aprili na amekuwa huko hadi sasa. Hakuna chakula , hakuna kitu. Tunajaribu kuwasaidia.”

Forum

XS
SM
MD
LG