Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 14, 2024 Local time: 09:35

Polisi Msumbiji wapambana na maandamano makubwa ya kupinga matokeo ya uchaguzi


Waandamanaji akirusha mawe wakati wakipinga matokeo ya uchaguzi huko Luis Cabral Maputo, Msumbiji Novemba 7, 2024. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko
Waandamanaji akirusha mawe wakati wakipinga matokeo ya uchaguzi huko Luis Cabral Maputo, Msumbiji Novemba 7, 2024. Picha na REUTERS/Siphiwe Sibeko

Polisi wamefyatua risasi na gesi ya kutoa machozi wakati mamia ya waandamanaji wakiingia mitaani kupinga uchaguzi wa Msumbiji.

Makundi ya kutetea haki yanasema takriban watu 18 wameuwawa katika operesheni hizo za polisi katika maandamano yanayopinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 9 ambao umeongeza utawala wa chama cha Frelimo kwa miongo mitano.

Vyama vya upinzani, makundi ya jamii na waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi haukuwa haki na matokeo yalichujwa.

Msemaji wa Frelimo hakujibu ombi la kumtaka kutoa maoni.

Siku ya Alhamis imepewa jila la “Siku ya Uhuru” katika vipeperushi vilivyosambazwa katika mitando ya kijamii na mgombea urais Venancio Mondlane.

Mondlane anaongoza ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana waliokata tamaa na kutokea wa pili katika katika matokeo rasmi ya uchaguzi, lakini amedai kuwa ameshisha.

Vikosi vya Usalama vilifanya doria katika barabara kuu inayoingia katika mji mkuu siku ya Alhamis.

Shirika la habari la Reuters limesema makundi ya watu yamekuwa yakijaribu kuingia katika jiji hilo kwa miguu.

Waandamanaji wakiwa wamebeba mabango yakiwa na picha ya mgombea huru wa urais Venancio Mondlane
Waandamanaji wakiwa wamebeba mabango yakiwa na picha ya mgombea huru wa urais Venancio Mondlane

Kila mahali katika jiji, makundi ya waandamanaji yamekuwa yakichoma moto mataili na kuweka vizuizi barabarani.

Afrika Kusini imefunga mpaka wake mkubwa siku aya Alhamis kwa sababu za kiusalama, na kuwashauri raia wake kutofanya safari zote zisizokuwa na umuhimu kwenda Msumbiji.

Kampuni ya usafirishaji ya Afrika Kusini siku ya Alhamis imesimamisha shughuli za bandari nchini humo.

Baraza la Katiba wiki hii limeiamrisha tume ya uchaguzi kutoa maelezo kwa nini kumekuwa hakuna uwiano wa idadi za kura zilizohesabiwa katika uchaguzi, kulingana na barua iliyoonekana kwa shirika la habari la Reuters.

Msemaji wa Tume ya uchaguzi hakuweza kujibu kwa haraka ujumbe uliotaka maoni yake.

Forum

XS
SM
MD
LG